Mkoa wa mwanza
Historia Sekretariati ya mkoa
Sekretariati ya mkoa asili yake ni sera ya Taifa ya kupeleka madaraka karibu na wanachi ya Mwaka 1972.Kimsigi sera hii ilisogeza madaraka ya kiwizara mikoani na kutekelezwa chini ya Mkurugenzi wa Maendeleo wa mkoa (RDD).Muundo huu wa kiutawaala mkoani ulihitimisha mamlaka za asili zilizokuwepo.
Katika muundo huu Wataalamu waliajiriwa na wizara mama na RDD aliajiri watumishi mwisho ngazi ya mshahara GS2.
Mnamo mwaka 1996 ofisi ya RDD ilisitishwa na nafasi yake kuchukuliwa na ofisi ya Katibu Tawala wa mkoa chini ya ofisi ya Waziri mkuu(OW-MKUU).Sheria Na.19 ya Mwaka 1997 ya Tawala za Mikoa ilihalarisha uazishwaji wa Ofisi ya Katibu Tawala wa mkoa chini ya Ofisi ya Waziri mkuu.Mnamo Novemba 1998 Wizara ya Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa iliundwa na ofisi ya Katibu Tawala kuwa Chini ya Wizara hiyo.
Hata hivyo mnamo januari 2000 Wizara ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa ilihamishiwa ofisi ya Rais na kujulikana kama OR-TAMISEMI(PORALG).
Mwaka 2002 muundo wa Tawala za Mikoa wenye idara ulifanyiwa tathmini na kuwa “CLASTA”ambazo ziliwajibika kwa Katibu Tawala.
Katika awamu ya nne ya Uongozi januari 2006 TAMISEMI ilirudishwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Lengo la Mabadiliko haya yote ilikuwa ni kupeleka madaraka karibu zaidi na wananchi .Hata hivyo ofisi ya RDD na serikali za mitaa zilizorejeshwa Mwaka 1984 zilikuwa na mwingiliano(Mgongano) kwenye shughuli zake za kila ziku kwa kuwa zote zilikuwa zinatekeleza sheria Na.7 na Na.8 ya mwaka 1982 na kwa kufanya hivyo kulikuwa na athari za kimaendeleo.Kwa upande mwigine mchakato huu ulikuwa na manufaa kwani wataalamu walipelekwa kwenye serikali za mitaa na kuzijengea uwezo wa kiutendaji.
Mnamo mwaka 2011 kwa mara nyingine muundo wa Tawala za mikoa wenye KLASTA ulifanyiwa tathmini na kuundwa “SEHEMU”(Section) na “VITENGO”(Units) kama ifuatavyo:-
- Seksheni ya Utawala na Raslimali watu.
- Seksheni ya Mipango na Uratibu.
- Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji.
- Seksheni ya Afya na Ustawi wa Jamii.
- Seksheni ya Miundo Mbinu
- Seksheni ya Menejimenti za Serikali za Mitaa.
- Seksheni ya Elimu.
- Seksheni ya Maji.
- Kitengo cha Fedha na Uhasibu.
- Kitengo cha Ukaguzi wa hesabu wa ndani.
- Kitengo cha Menejimenti ya Manuuzi.
- Kitengo cha Sheria.
- Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
- Ofisi za Wakuu wa Wilaya.
Anuani zetu
|