TV1
Kuhusu Sisi
TV1 ni sehemu ya Modern Times Group (MTG), watangazaji wa kimataifa wa burudani wanaoongoza na wanaoendesha shughuli zao katika mabara manne tofauti. Ili kujua zaidi, tembelea tovuti ifuatayo: www.mtg.se.
TV1 Tanzania ilianza kurushwa hewani tarehe 10 Januari 2014 ikiwa na shauku na hamasa ya kubadilisha mazingira ya vyombo vya habari nchini. Kwa mara ya kwanza, chaneli ya TV ya Kitanzania inawaletea vipindi vya viwango vya juu kabisa bila malipo yoyote. Kuanzia vipindi vilivyoandaliwa na studio maarufu za kimataifa hadi vipindi vya kipekee vyenye maudhui kutoka Afrika pamoja na vipindi vinavyotengenezwa hapahapa nchini, TV1 ina burudani ya kila aina kwa ajili yako na familia yako. Ili kutupata, tegesha dikoda yako ya StarTimes katika chaneli 103. Furahia vipindi vyetu bila malipo.
Timu kabambe ya wataalam wazawa na wa kimataifa ndio waendeshaji wa chaneli hii. Timu hii, ikifanyia kazi kutoka mjini Dar es Salaam katika studio ya TV yenye viwango vya hali ya juu, inatayarisha miundo mipya ya vipindi kutoka hapahapa nyumbani kila wakati.
Matarajio Yetu
Kuwa vinara katika kuwaletea uburudishaji usiokuwa na malipo nchini Tanzania kwa kuwafikishia watazamaji maudhui ya Kiafrika na ya kimataifa yenye viwango vya hali ya juu na kutayarisha vipindi bora vya kutoka hapahapa nyumbani. Vionjo vya nyumbani vyenye viwango vya kimataifa.
Jukumu la Kampuni kwa Jamii
Tumejikita katika kuwa kampuni inayostawi yenye lengo la kuwa na athari chanya kwa mazingira yetu na maendeleo ya kibiashara yenye maadili na endelevu yanayoshirikisha jumuiya zetu. Kwa maana hii, tuna kusudio la kuboresha hali ya maisha ya jamii tunakoendeshea shughuli zetu. Kazi zetu katika suala hili zinagawanyika katika miradi miwili tofauti, wa kwanza ni “Reach for Change” na wa pili ni “MTG United For Peace”.
Contact us
Viasat 1 Tanzania Ltd.
Mikocheni A Ind. Area, Plot No. 81.
P. O. Box 31119, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 658 455 121
For information and feedback email: info@tv1.co.tz
For advertising with TV1 email:: sales@tv1.co.tz